Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Happyness W. Seneda asubuhi ya leo amekwenda Kiluvya kwa Komba kuwatembelea na kuwafariji walio ondokewa na wapendwa wao kufuatia mvua kubwa zilizonyesha!!
Tumepoteza watu wawili kwa takwimu za mpaka leo asubuhi.
1. Mtoto Theddy mwenye umri wa miaka 8
2. Kijana Issa Ally mwenye miaka 28 aliyekwenda kumuokoa Theddy. Kijana huyu alihitimu mafunzo ya jeshi la akiba mwaka jana na alipata ajira SuMA JKT.
Mwili wa Theddy umeshapatikana, juhudi zinaendelea kuupata mwili wa Issa.
Mungu wa mbinguni azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amen.
Hakika ni msiba mzito, kama wilaya tutashirikiana katika kila jambo.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa