NIMEFURAHISHWA NA MMLIVYOJIPANGA KISARAWE CHATANDA NA ZAINABU
KISARAWE.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mambo Mengi ya kimaendeleo hususani katika Wilaya ya Kisarawe Pwani 08/05/2025.
![]() |
![]() |
Akizungumza kwenye ziara Pwani Wilaya ya Kisarawe Chatanda Amesema Sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu mbalimbali pamoja uwezeshaji Wananchi kiuchumi Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan imekua madhubuti sekta hizo ili kuwaondolea adha wananchi wa Kisarawe,
Chatanda Amewasihi wananchi wa Kisarawe kujitokeza katika kuboresha Taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura litakapowafikia kwa awamu ya pili, sanjari na kujitokeza kwenye zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka Huu kwa kuwa Uchaguzi upo na waachane na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa ambao si wazalendo wa Taifa hili.
![]() |
![]() |
Nae Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Mhe Zainabu Vullu amesema kuwa ziara ya Mhe Chanda na Timu yake Kisarawe Ni Fahari maana kuja Kuona mafanikio ya Awamu ya sita Chini ya Rais Dkt Samia katika Wilaya ya Kisarawe,
![]() |
![]() |
Ziara hiyo ya siku moja imefanyika katika kata Saba za Kisarawe, masaki,msimbu,mzenga,chole na maneromango kwa kuwatembelea wananchi na wanachama mbalimbali.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa