NIMERIDHISHWA NA MAENDELEO YA VETA KISARAWE-RWEZIMULA
Kazimzubwi Kisarawe
Naibu katibu mkuu wizara ya elimu
Franklin jasson rwezimula amefanya ziara katika halmashauri ya wilaya ya kisarawe katika ujenzi wa VETA ya kazimzubwi kujionea maendeleo ya ujenzi wa VETA hiyo .
Katika ziara yake ya kutembelea VETA zote zinazo jengwa hivi sasa kwa maagizo ya Dkt Samia Suluhu Hassan akipendelea kila wilaya kuwa na VETA inayo toa mafunzo ambayo ni msaada kwa wananchi wa maeneo hayo.
Pia amepongeza speed ya ujenzi wa majengo hayo japokuwa halmashauri ya kisarawe ili kuwa ya mwisho mwisho kupokea mradi huo na wao wamewapita walio tangulia kupokea mradi.
Lakini amemuomba mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh Fatma Almas Nyangasa kusaidia kwenye mambo ambayo yanachelewesha ujenzi wa VETA hiyo kama vile kuwepo na karavati katika sehemu korofi inayo sababisha kuto fika kwa wakati Na maji ya uhakaki kwa ajili ya matumizi ya kipindi cha ujenzi na baada ya kukamilika kwa ujenzi
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa