NMB Yakabidhi Madawati Wilaya Ya Kisarawe
Benki ya NMB Tanzania imekabidhi madawati mia moja katika Wilaya ya Kisarawe kwa ajili YA Matumizi kwa shule mbili za Sekondari ya Masaki na Mfuru zilizopo Wilaya ya Kisarawe.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari vya Masaki na Mfuru Mkurugenzi wa masuala ya serikali wa benki ya NMB bi………….alimkabidhi madawati Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amesema Benki ya NMB imeweka kipaumbele kushirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.
‘’Tulipopata maombi yenu,tulifarijika na kuamua mara moja kuja kushirikiana na ninyi ili kuwa chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu.Madawati tunayokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikiksha jamii inafaidika kutokana na faida tunayopata.Benki ya NMB imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia sekta ya elimu afya pamoja na kufariji jamii katika vipindi mbalimbali kama mafuriko,matetemeko na ajali mbalimbali zinazogusa jamii’’Amesema Bi Aneth Kwaya
Wakati akipokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo ameishukuru benki ya NMB kwa msaada huo ambao utakuwa chachu kubwa kwa matokeo mazuri kwa wanafunzi .Pia aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuleta matunda
‘’Zero haikubaliki,hatuitaki zero! Hatuongei tu bali tunamaanisha,Walimuwanafanya kazi nzito kuwafundisha,serikali inafanya kazi ya kipekee na benki ya NMB ikaona iweke mkono wake ili kuwabariki wanafunzi ili mazingira yenu ya kusoma yawe mepesi. Kwa hiyo ninyi kama wanafunzi mna deni zito sana la kulipa na deni hilo mtalilipa pale tu mtakapofanya vizuri darasani na kufaulu’’ Amesema Mheshimiwa Jokate.
Katika makabidhiano hayo Benki ya NMB imekabidhi jumla ya madawati mia moja yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni tano ambapo shule ya Sekondari ya Masaki imepata madawati hamsini na Shule ya sekondari ya Mfuru imepata madawati hamsini.
Hafla ya makabidhiano pia imehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata ya Masaki na Marumbo Mhe.Pili Chamgui na Mhe.Mayasa S. Yange, Katibu Tawala wa Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba,Kaimu Mkurugenzi Ndugu Patric Allute,Afisa elimu Sekondari bi Generosa Nyoni na Maafisa wa Benki ya NMB Tawi la Kisarawe wakiongozwa na Meneja wa benki hiyo Ndugu Sumka
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa