NMB YATOA VIFAA VYA UJENZI KISARAWE
KISARAWE PWANI
Banki ya NMB tawi la Kisarawe Kanda ya DAR ES SALAAM Leo 16.11.2023 imetoka VIFAA VYA Ujenzi Katika Halmashauri ya Wilaya Kisarawe
Akizungumza wakati wa Kutoa Vifaa hivyo meneja wa Kanda ya DAR ES SALAAM Ndg DISMAS PROSPER Alisisitiza Kuwa Benki ya NMB imekua karibu mno na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Kwa muda mrefu Katika kuchangia Maendeleo,
"*Sisi kama benki ya Maendeleo tupo hapa kuchangia Maendeleo na Kwa Kisarawe tumekua Wadau wakubwa Kwao Katika Elimu, Afya ,n.k Katika kuchangia Maendeleo alisisitiza Ndg DISMAS
Nae Mkuu wa Wilaya Kisarawe Mhe FATMA NYANGASA alishukuru Kwa benki Hiyo kuchangia Maendeleo hasa ya Elimu Kisarawe,
*" Binafsi nafarijika Kuona nyie Banki ya NMB mmekua Wadau wakubwa Kisarawe Katika kuchangia Maendeleo alishukuru Mhe NYANGASA,
Akizungumza Kwa Katika hafla Hiyo mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC alisema Kuwa mchango huo wa Mabati Kwa Shule za Kisarawe umekuja wakati muwafaka hasa kutokana na uhitaji wake Kwa Shule hizo za Kisarawe
Jumla ya bati 600 zimetolewa Kwa Shule za Kisarawe za Panga la mwingereza,Titu, kibasila,mtunani na vilabwa Vifaa hivyo vina Dhamani ya Shilingi million ishirini na Nane na laki Mbili(28,200,000)
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa