PINDA,KIZWEZWE, BEATRICE WAWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA ZA NANENANE KUINUA KILIMO, UFUGAJI NA UVUVI KISARAWE
Na
MWANDISHI WETU
Maonesho ya nanenane Kanda mashariki katika mkoa wa Morogoro, Tanga,Dar es saalam na Pwani yanayofanyika Mkoani Morogoro yamefunguliwa Leo 01.08.2023 na Waziri Mkuu Mstafu Mhe Mizengo Pinda,
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Mhe Pinda alisisitiza jamii kulima na Kulinda chakula huku wakitumia Teknologia katika Kilimo cha Kisasa na mkakati ili kupata faida zaidi na Kulinda Chakula nchini,
"Ikiwa Watanzania walio amua kulima basi wakilima Kwa Kutumia Teknologia ya Kisasa katika mazao ya kimkakati basi itakua Vyema na taifa litakua na hifadhi zaidi ya Chakula hasa vyakula vinavyohimili ukame Kwa badhii ya sehemu ambazo zinapata mvua ndogo alisisitiza Mhe Pinda"
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Bi Betrice Dominic alitoa wito Kwa wakaazi wa Kisarawe na Tanzania Kwa ujumla Kutumia fursa za uwepo wa ardhi zenye rutuba kulima Kwa kasi zaidi kupata maendeleo ya chakula na Kilimo,
"Kisarawe Ina ardhi nzuri Sana hasa Kata za Marui, Mafizi,Kurui na Mzenga na serikali imetoa madawa Kwa ajili ya kusapoti Kilimo ,mifugo basi shime tumieni fursa hiyo"
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Mhe Zuberi Kizwezwe aliwataka Wanakisawe kuwatumia watalaamu wa Kilimo na Mifugo waliopo kata na vijijini katika kupata ushauri wa kitaalamu kupata usalama wa Kilimo na chakula,
"Wananchi wa Kisarawe katika zile kata ambazo zinalima basi ni Vyema wakawatumia watalaamu Wote hao katika kupata msaada wa kuboresha Kilimo cha Kisasa"
Nae afisa Kilimo Ufugaji Kisarawe Ndugu Sadiki Msangi aliwaomba watalaam wa Kilimo na Mifugo Nk kuwa karibu wa Wadau katika kutoa ushauri elekezi ili kufanikisha Kilimo ili kuongeza uzalishaji wenye Tisha.
Maonesho ya nanenane Kanda mashariki mwaka huu yamekuja na kauli mbiu Vijana na Wanawake ni
Msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.
Unaweza pata taarifa mbali mbali kuhusu halmashauri ya Wilaya ya kisarawe kwa kusikiliza vide bofya hapo--->[MAKALA KISARAWE]https://youtu.be/7cUvoR318lA
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa