Plan Internationa Kisarawe Yakabidhi Pikipiki Kwa Chombo Cha Watumia Maji kijiji cha Kurui na Mtakayo
Shirika la misaada la Plan International Wilaya ya Kisarawe imekabidhi pikipiki kwa chombo cha watumia maji wa kijiji cha mtakayo na kurui kata ya kurui kwa ajili usimamizi na udhibiti wa matumizi ya maji.
Akikabidhi pikpiki hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ndugu Mussa Gama, Meneja wa Plan internation Kisarawe Ndugu Philipina Kihupi amesema wanakabidhi pikipiki ikiwa ni ahadi ya waliyoitoa ya kutoa chombo cha usafiri kwa watumiaji maji wa kijiji cha kurui na Mtakayo.
Katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kisarawe Ndugu Mussa Gama ameshukuru msaada uliotolewa na Plan kwani utasaidida kwa kiasi kikubwa tatizo la usimamizi wa matumizi ya maji kwa wananchi
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe akiwemo Mhandisi wa maji wa Wilaya Injinia Majd Mtili ,Wataalam wa maji na maofisa kutoka idara ya maendeleo ya jamii.

Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa