RAS PWANI AFURAHISHWA NA MAONESHO YA NANENANE BANDA LA KISARAWE AHIDI KUFIKA KUJIONEA KWA VITENDO
MOROGORO
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Pili H. Mnyema amewataka wafugaji kuacha kufuga kwa kuhamahama sambamba na kufurahishwa na mafanikio ya Kisarawe katika Banda la nanenane mwaka 2025,
Hayo ameyasema jana tarehe 07/08/2025 alipotembelea eneo la maonesho ya halmashauri ya wilaya ya Kisarawe (Nanenane) ambapo alishangazwa na mafanikio ya Kisarawe hasa katika ufugaji ngombe na Kilimo Cha mananasi,
![]() |
![]() |
![]() |
Aidha amewasisitiza wataalam kuendelea kuwahamasisha wafugaji kulima mashamba ya malisho na kutumia mifugo bora ya ng'ombe na mbuzi ili kuwa na ufugaji wenye tija katika jamii
"Ili kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji, wafugaji muache ufugaji wa kuhamahama na wataalamu endeleeni kuwa karibu Sana na wakulima katika kuwapa Msaada wa kitalamu" amesisitiza Bi. Pili.
![]() |
![]() |
![]() |
Nae Mkulima Bora 2024 Ndg Jumanne S Sama anaeshiriki maonesho haya) amesema siku hizi wanajitahidi kutumia mashamba yenye udongo asili. Aidha wanaendelea kuelimishana wao kwa wao ili kuwa na ukulima wenye tija na faida,
![]() |
![]() |
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa