RAS PWANI ARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO KISARAWE
Kisarawe PWANI.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Ndugu RASHIDI MCHATTA amefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo leo 28/03/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, na kuzungumza na Walimu wa Shule ya Kimani wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, NDG BEATRICE DOMINIC,
Katika ziara hiyo Katibu Tawala Mkoa alianzia ziara yake Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambako alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA kabla ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali Kiwilaya, Taarifa iliyosomwa mbele yake na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe juu ya Miradi anayotembelea ya Jengo la Utawala,Bweni na Bwalo shule ya Sekondari ya Kimani,
Aidha, katika ziara hiyo, Katibu Tawala Mkoa, Ndugu. RASHIDI KASSIM MCHATTA amefurahishwa na ushirikiano baina ya Watumishi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi.
Pia ametumia fursa hiyo kueleza vipaumbele vyake kuwa ni kuhakikisha Halmashauri inaimarisha ukusanyaji mapato ya ndani, Kuimarisha utoaji huduma za utalii na kutunza miundombinu ya utalii, kuimarisha na kuboresha utoaji huduma kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, kuboresha miundombinu ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na wan je, kuboresha utoaji huduma za ugani kwa wakulima na wafugaji na mwisho ni uboreshaji wa fursa na miundombinu ya uwekazaji wa viwanda, kwani shughuli hizi za ni shughuli mama katika ukuzaji uchumi wa Halmashauri, Mkoa na Taifa kwa ujumla alisisitiza Ndugu. RASHIDI MCHATTA
Aidha Katika ziara Hiyo pia alikagua Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara inayojengwa kwa kiwango Cha Lami kutoka Kisarawe mjini Kuelekea kitongoji Cha Kimani kwa umbali Mita 500 sawa na Nusu kilomita.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa