Tarehe 10/12/2021 Mkuu wa Mkoa Mhe. Abubakari Mussa Kunenge ametembelea miradi ya ujenzi wa Madarasa ya UVIKO 19 Katika Wilaya ya Kisarawe.Katika ukaguzi huo Mhe. Kunenge alipongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi na kutoa maelekezo ya kukamilisha madarasa hayo kabla ya wakati kama ilivyoelekezwa na Serikali.Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Nickson John alitoa maelezo juu ya utekelezaji wa Miradi ya uviko 19 na hatua iliyofikia kisha kuikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa.Ziara ya Mkuu wa Mkoa aliambatana na RAS, wataalamu toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa