kamanda wa tasisi ya kupambana na kuzuia rushwa kisarawe (Takukuru) Ndg Alfeo Silungwe Ameitka jamii kufichua na kuwataja watu wote wale wenye mamla ya kusimamia mali za umaa ambao hujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma kwani hiyo nayo ni rushwa ambayo hurudisha nyuma maendeleo katika jamii yetu ya kisarawe
Akizungumza hayo katika uhamasishaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi kola na sekondari ya Mzenga kisarawe
Alisema ‘’ndugu zangu wanakisarawe rushwa ni adui wa maendeleo na haki hivyo nakuombeni sana ili kupata maendeleo tunayoyataka ni muhimu kuwafichua wala rushwa katika jamii zetu ambao wanasimamia miradi ya jamii kama shule,zahanati, miradi ya kijiji na nyumba za watumishi ‘’ alisisitiza silungwe
Rushwa imeendelea kuwa kikwazo kikubwa katika jamii yetu ya sasa kutokana na jamii kubwa hasa ya vijijini kutokua na mwamkoa mkubwa wa utambuzi wa kuwabaini na kubaini matendo na matukio ya rushwa katika jamii
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa