Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania kupitia kwa Eng Dr Victoria Helman kimeuhakikishia umma wa kisarawe kuwapatia majengo yenye ubora katika kuhakikisha mwanzo mpaka mwisho wa majengo hayo yanakua na ubora unaoutakiwa kwa mujibu wa viwango vya ujenzi wa majengo ya serikali ya Tanzania,
Akizungumza kisarawe leo Eng Dk Helmani amesema wao kama Tawa kwa mamlaka walio nayo na Dhamana waliyopewa na watanzania watahahkikisha suala la ubora na ufanisi wa kupata ubora wa madarasa ya shule ya maluumu ya wasichana inayoyengwa Tarafa ya Sungwi Kata ya Kibuta Kijiji cha Mhaga ni la lazima na muhimu kwa mustakabali wa wasichana wote wa kitanzania
‘’Suala la kuhakikisha kuwa Tawa tunasimamia ubora wa kandarasi ya majengo haya ya shule ya wasichana kisarawe ni lazima kwa kizazi cha leo na kesho maaana hii shule ikimalizika itakua sio ya wanakisarawe pekee bali ni ya kila mtanzania mwenye sifa ya kusoma shule hii kwa ngazi ya kidato cha kwanza mpaka cha sita,’’ alisema eng dk Helman
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kisarawe Ndg Mussa Gama aliwashukuru Tawa kwa moyo wa kizalendo kwa kuja kujitolea kuja kusimamia kitalaam ujenzi wa shule hii ya kisasa ya wasichana kisarawe,
‘’Binafsi mimi na watumishi wenzangu wa hapa kisarawe tunawashukuru na kutambua mchango wenu wa kitalaam katika kampeni hii ya TOKOMEZA ZERO KISARAWE Imani pia mtashirikiana na watalam waliopo hapa Halmashauri katika kupata majengo yalio bora na salama kwa ujumla pamoja na kubadilishana uzoefu wa taluma ya kusimamia majengo ya serikali.’’ Alimalizia Ndg Gama
‘’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa