"UFAULU WA MASOMO KWA MTOTO WA KIKE NI FAHARI YETU-DKT JAFO"
Na
Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amesema kuwa mafanikio ya Mtoto wa kike katika masomo ni Fahari Sana kwa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan,
Akizungumza Wakati wa Mahafali kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige A leo 26/09/2023 alisema kuwa Miongoni mwa Fahari kwa Mhe Dkt Samia ni kuona mafanikio ya Mtoto hasa Wa kike katika Elimu na Nyanja mbalimbali za maendeleo Tanzania,
"Ndugu zangu na Watoto wangu Leo mnamaliza Elimu ya Msingi serikali yenu tayari imeshawandalia Mazingira mazuri ya kusoma elimu ya Sekondari hivyo nendeni katimizeni ndoto zangu ili kumheshimisha Mhe Dkt Samia pamoja na Wazazi wenu" alisisitiza Mhe Dkt Jafo
"Uridhi mzuri kwenu watoto ni Elimu na sio vinginevyo hivyo mjitahidi Sana kuwa makini mnapokua katika kusoma hasa Masomo ya Sekondari" alisisitiza Mhe Dkt Jafo
Mahafali ya shule Msingi Chanzige A ni Mara ya sita tokea kuanza kwa shule hiyo kata ya Kisarawe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa