Ujenzi Wa Kituo Cha Afya Mzenga Waendelea Kwa Kasi.
Tarafa ya mzenga iliyomo wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani imezidi kuchanja mbuga katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zilizo bora kwa kuendelea kutekeleza ujenzi wa kituo bora cha afya
Katika ujenzi huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni mia tano 500,000,000/= zilizotolewa na serikali kuu ambazo zitafanikisha uboreshaji na ujenzi mpya wa miundombinu wezesh itakayosaidia kuongeza huduma zitolewazo hapo kituoni.
Ujenzi wa kituo hiki ulianza Mwanzoni mwa mwaka huu na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni mwaka huu,ujenzi umefikia kiwango cha mwisho wa ukamilkaji wake wa ujenzi ambapo jumla ya majengo matano yamejengwa
Miundo mbinu ya afya iliyojengwa katika kituo cha afya cha Tarafa ya Mzenga inajumuisha Maabara,wodi ya wazazi,chumba cha upasuaji ,chumba cha kuifadhia maiti pamoja na nyumba ya mganga .Pia kituo kitakuwa na vifaa tiba vyote vinavyohtajika katika huduma zitolewazo hapo.
Wilaya ya kisarawe ina jumla ya vituo vinne vya afya vya Tarafa ya Chole,Maneromango.Masaki pamoja na Mzenga ambapo zoezi ya k
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa