UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO KITUO CHA AFYA MANEROMANGO WAENDELEA KWA KASI
Kituo cha Afya Maneromango kimepatiwa jumla ya fedha za Kitanzania zipatazo milioni mia tano(500,000,000/=) ambazo zimetolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ukarabati wa Majengo ya zamani na ujenzi wa majengo mengine mapya matano(5),Majengo hayo ni pamooja na Nyumba ya Mganga,Jengo la Upasuaji,Wodi ya Wazazi,Jengo la kuhifadhi Maiti na Maabara.
Majengo haya yapo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi,Nyumba ya Mganga ipo hatua ya Gego,Wodi ya wazazi na Jengo la Upasuaji yapo hatua ya kuwekwa “ring beam”,Maabara imeshawekwa “ring beam” na Jengo la kuhifadhia Maiti lipo hatua ya Msingi.
Aidha majengo haya yote yatakamilika kabla ya tarehe 31/12/2017.HABARI PICHABOFYA HAPA
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa