UMOJA, NIDHAMU, HEKIMA NA USHIRIKIANO WA DC,DED KISARAWE WAMFURAHISHA DR MARY MWANJELWA
Katika Kufikia Malengo ya Utawala Bora kwa Watumishi na Wananchi wa Kisarawe uwepo wa Umoja,Nidhamu, Hekima na Ushirikiano wa Mkuu wa Wilaya na ,Mkurugenzi Mtendaji Kumemfurahisha na kuwa ni Jambo la Kuigwa kwa Viongozi Wengine wa Halmashauri na Wilaya Nyengine Nchini
Hayo yametamkwa na Mhe Dr Mary Mwanjelwa (MB) Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipokua akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambapo Alipata Wasaa wa kusikiliza Kero na Changamoto Mbalimbali Wanazokumbana Nazo Watumishi hao wa Halmshauri na Serikali Kuu katika Kuwahudumia Wananchi Katika Sehemu za Kazi
‘’Umoja Huu wa Viongozi Hawa Vijana wa Kisarawe ni wa Kuigwa Kwani Huko Sehemu Nyengine za Halmashauri Hali Sio Nzuri Kwani Utakuta DC na DED Kila Mtu na lake lakini Hapa Kisarawe Hali Tofauti Kambsa Kwani Kila Mmoja Yupo na Zake za kutatika Kuwahudumia Watumishinna Wananchi Nasema Chapeni Kazi Hapana Kulala awamuu Hii ya Tano sio ya Mchezo Mchezo Rais Anafurahihwa na Utendaji Wenu wa kazi’’ alisema Dr Mwanjelwa
Aidha Dr Mwanjelwa alitoa Wito kwa Mafisa Watumishi Wote Tanzania Kuharakisha Kuwasilisha Tarifa za Watumishi ambao Mpaka sasa Hawajapandishwa Vyeo na kubadilishwa Majukumu yao kwa Mujibu wa Sheria kwa Wale ambao Wanastahiki Kupata Hizo Stahiki Kwani wao Kama Wizara Wameshalitatua Tatizo ambalo Lilikuapo kwa Upande wa Mkoa wa Pwani ila kwa sasa tumelitatua tatizo hili la mpokeaji tarifa ,
‘’Maafisa Utumishi Wote Nchini Nawagiza Kupeleka Tarifa za Watumishi Mnaowasimamia Wizarani ili kupata stahiki zao kama kupanda vyeo na Recogarization kwa watumishi ambao wanastahiki ili Wapatiwe Haki zao Ndani ya Siku 21 tu’’ alisema Dr Mwanjelwa
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa