Katika kuunga mkono Jitihada za Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi na kuwatatulia kero zao kwa vitendo na weledi na kwa wakati Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo amechukizwa na mwenendo mbaya wa matokeo ya utoro,uzembe,zero kwa badhii ya shule za sekondari za wilaya ya kisarawe kwa wanafunzi,
Amemuagiza Afisa Elimu Sekondari kusimamia haraka kero hiyo kwa weledi wa matokeo mazuri ya walimu wilaya hiyo sambamba na kutatua changamoto zao kwa wakati ili waweze kutoa matokeo mazuri katika elimu hasa kwa vijana na wanafunzi wa kike
Maaana serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya miundo mbinu bora na imara kwa sekta ya elimu kisarawe ikwemo ujenzi wa miundombuni ya madarasa,mabweni ya wanafunzi wa kike na kiume ,vyoo, ofisi,na nyumba za walimu na ofisi kwa shule mbalimbali kisarawe alisema Eng Ndikilo ‘’
Haiwezekani shule ina walimu wengi majengo mazuri na kila aina ya kitendea kazi inavyo kisha inatoa matokeo ya ZERO kwa wanafunzi wake hapana hii haikubaliki kabisa nakuagiza afisa elimu fanya uhamisho wa ndani haraka kwa walimu hapa kisarawe ili kuboresha ufanisi wa kazi za walimu hapa haraka sana’’ alisema Eng Ndikilo
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa