Jumla ya ekari mia mbili za ardhi zitatumika kujenga chuo cha Kisasa cha mafunzo mbalimbali ya elimu ya ustadi na ufundi kata ya kazimzumbwi kisarawe kitakacho simamiwa na chuo cha ufundi na ustadi (VETA) hayo yote yakiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa wananchi wa kisarawe
Akizungumza wakati wa utambulisho wa Bodi ya VETA kwa Uwongozi wa Wilaya ya kisarawe Mkurungenzi mtendaji wa Wilaya Kisarawe Ndg MUSSA GAMA Alisema kisarawe ina maeneo mengi ambayo yanahitaji kuendelezwa kwa uwekezaji wa kilimo,ujenzi wa viwanda pamoja na uwekezaji wa sekta elimu kama huu wa ujenzi wa chuo cha VETA unaotaka kuanza hapa kwetu kwani ndio uwekezaji wenye tija na manufaa kwa wana kisarawe
’’unapowekeza katika elimu unakua unakomboa taifa kwenda katika mafanikio ya kisasa ya ya kielimu hasa haya ya VETA na Tehama yanayokusudiwa kuanza kwetu maana yatakua na manufaa kwa taifa na kisarawe yote’’ alisema Gama
Alishukuru VETA kwa kukubali kujenga chuo hicho cha kisasa kisarawe kwani jamii hiyo itagomboka kwa kupata elimu na kupelekea kuondokana na umasikini wa maisha kwani jamii kubwa itakua na fursa nyingi za kielimu na taluma na ujuzi pamoja na vipaji mbalimbali ambazo zimefundishwa katika chuo hicho cha VETA kisarawe.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa VETA Dkt Pancra Bujulu alishukuru uwongozi wa wilaya ya kisarawe kwa kukubali kuwapatia eneo hilo ambalo watalitumia kwa ufanisi na mafanikio kama ambavyo imekusudiwa kwa jamii hiyo ya kisarawe na taifa kwa ujumla kwani wao kama VETA kwa sasa fedha za mradi huo tayari zipo tayari kwa ajili ya utekelezaji tu wa ujenzi huo wa chuo kisarawe
‘’kwa niaba ya bodi ya VETA tunawashukuru sana uwongozi wa kisarawe kwa umoja wenu na ushirikiano katika kuwahudumia wananchi wenu katika kuwapatia huduma bora wanakisarawe sisi tunawahidi kukamilisha mradi huu kwa wakati’’ alisisitiza Dkt Bujulu
Mradi huu VETA utakapo kukamilika kujengwa kisarawe unategemewa kutoa mafunzo ya elimu ya Upishi,Ufundi Sanifu, Kilimo , Magari, Uwashi,Mapambo ,Mapishi,ushoni, Usafi,Mapokezi,Umeme, Sambamba na TEHAMA
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa