VIJANA KISARAWE WATUMIA MKOPO KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.
Vikundi viwili vya vijana vya Kata ya Kisarawe na Vihingo vinavyojulikana kama MAPAMBANO na UWAPIKI vimetumia mkopo wa shilingi 12,000,000/= kwa kununua pikipiki 6 ambazo zitatumika na vikundi hivyo katika shughuli za kujiongezea kipato.
Fedha hizo zilitolewa na Halmashauri katika kutekeleza majukumu yake ampapo inatakiwa kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kuwezesha kiuchumi vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.
Akikabidhi pikipiki hizo Katibu Tawala Wilaya Ndg Mtela Mwampamba aliwaasa vijana kuwa pikipiki hizi ni mali yao na zinatakiwa zitumike kwa kazi zilizokusudiwa ili ziwaongezee kipato na kuweza kurejesha mkopo kwa wakati na sio kwamba ziende kutumika kwenye shughuli nyingine za kiharifu ,pia aliwaasa kufuata sheria zote za usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwa pamoja na kujisajili kama vyombo vya Usafiri na usafirishaji
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa