*WALIMU WA AWALI NA MSINGI NI WAZURI KUIBUA VIPAJI VYA TEHAMA NA HISABATI-MWL SAIDI*
NA
Kisarawe Pwani
Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Kupitia mradi wa Shule bora Kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza Wameandaa Mafunzo Kwa walimu Mahiri wa Somo la Hisabati lengo ikiwa ni kuboresha ufundishaji na ufunzaji ili kuongeza ufaulu Katika mitihani ya Taifa,
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Kisarawe minaki Mwezashaji wa Mafunzo kuhusu TEHAMA Mwalimu Khamis Saidi Alisema
*"walimu wa Awali na Msingi watakapo tumia vyema vishikwambi walivyonavyo Kwa kutumia Teknolojia iliyopo ndani yake Kwa Wana uwezo wa kuwasadia watoto kufaulu vyema na kuelewa Kwa umakini somo la Hisabati Kwa njia ya vitendo*" alifafanua Mwalimu Saidi
*"Kwa Ujumla walimu wa awali na msingi ni wazuri Sana wakitumika Katika kuibua vipaji vya watoto hasa tehama na Hisabati*" alimalizia Mwalimu Saidi
Mafunzo hayo ya Walimu kuhusu uboreshaji wa ufundishaji na ufunzaji wa umahiri wenye changamoto Katika somo la Hisabati Mkoa wa Pwani Wilaya Kisarawe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa