Mkuu wa mkoa wa Pwani mheshimiwa Dk Evarist Ndikilo ameamuru kuwashughulikia wavamizi na waharibifu wa hifadhi za misitu iliyotengwa kisheria kwa ajili ya hifadhi.
Amri hiyo ameitoa hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya Mkoa ya siku ya upandaji miti iliyofanyika kwenye hifadhi ya misitu ya Kazimzumbwi inayopakana na kijiji cha Maguruwe katika Kata ya Msimbu Wilaya ya Kisarawe ambapo zoezi la upandaji miti lilifanyika.
Akiwahutubia mamia ya wakazi na watumishi waliojitokeza kwa pamoja katika zoezi la kupanda miti Dk Ndikilo amesema wananchi wanatakiwa kulinda misitu yetu kwa ajili ya maendeleo yetu kwani faida zitokanazo na misitu ni kubwa sana tofauti na faida za uharibifu wa misitu.
‘’ tuongeze juhudi za ulinzi katika rasilimali zetu kwani faida za misitu hii ni kwa ajili yetu na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam. Na hakuna mtu yoyote atakayeruhusiwa kuvamia na serikali ipo imara na wavamizi wote washughulikwe ipasavyo’’Alisema Dk Ndikilo
Aidha katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Pwani amewakumbusha wananchi faida za msigi za kuendelea kutunza misitu iliyopo mkoa wa wa Pwani hususani Wilaya ya kisarawe kwani ndiyo chanzo cha maji ya mito yanatirirka kwenda Mkoa wa Dar es salam na ndiyo inayonyonya hewa chafu ya viwanda vingi vilivyopo .
Vilevile ameongeza kuwa Misitu tuliyonayo ndiyo inahifadhi mmomonyoko wa udongo,inahifadhi viumbe hai na dawa za asili pamoja na kuwa sehemu ya mapafu ya kusafisha hewa tunayoitumia sisi viumbe hai.
Maadhimisho ya siku ya Upandaji miti kimkoa yamefanyika wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwamo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Happiness seneda na wakururugenzi Watendaji wa Halmashauri za Kisarawe,Mkuranga na Bagamoyo
By dkambanyuma
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa