WATAALAMU WA VIJIJI,KATA KISARAWE WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA FFARS
NA
Kisarawe Pwani
Halmashauri ya Wilaya Kisarawe kupitia kitengo Cha Fedha na Tehama wameandaa Mafunzo kwa ajili ya Kuwawezesha wataalam wa Elimu, Kilimo Mifugo na utendaji Kisarawe 07.09.2023.
Akizungumza na Wataalam hao Mkuu idara ya ya Utumishi na Utawala Ndug Baptista J. Kihanza aliwataka Wataalam hao kuonesha weledi wa kazi Pamoja na kutumia Vyema Umakini Mafunzo hayo ili kupata tija,
"Ndugu zangu Watumishi Wote mliopo hapa imani yangu mmepata na mnaendelea kupata mafunzo haya Ya FFARS ili kuleta Umakini Katika maeneo ya kazi alimalizia Ndugu Baptista Kihanza"
Mafunzo hayo ya siku moja kwa Wataalam wa Ngazi ya kijiji na kata kwa Maafisa watendaji kata, vijiji, na Walimu yamekuja yakiwa na lengo kuboresha ufanisi wa utendaji Kisarawe kwa shule,Vijiji na kata zote 17 za Kisarawe,
Kwa Upende wake msimamizi wa kitengo Cha TEHAMA Kisarawe Ndugu Joseph Kalolo aliema FFARS (Facility financial and Reporting System) Ni mfumo ambao ukifutwa Vyema na Watendaji kata na vijiji utaboresha usalama wa Kazi zao pamoja na kuboresha utalam Wenu na kuwatoa Shaka kuwa Mfumo huo sio mgumu Bali Mfumo unahitaji umakini
"Huu mfumo wa FFARS Facility financial and Reporting System unasaidia sana Ufanisi wa kazi Katika ngazi zenu Hivyo ni Vyema tukazingatia Umakini Katika Kuutumia alisisitiza Joseph Kalolo"
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa