Watu wenye ulemavu wilaya ya kisarawe wamekabidhiwa msaada wa vifaa saidizi vyenye jumla ya kiasi cha shilingi milioni arobaini ambavyo vitawasaidia katika kupambana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zina waathiri katika ufanisi wa ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.S
Katika zoezi hilo ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemeni Jafo amekabidhi vifaa hivyo kwa watu wenye ulemavu tukio lililofanyika kwenye uwanja wa stendi kuu ya Wilaya ya Kisarawe. Walemavu wamepatiwa wheel chairs 40,Trycicle 15 na white canes 100.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa ndugu Ummy Nderiananga amesema baada ya kuwapa vifaa watu wenye ulemavu, tusogee mbele kuwakwamu kiuchumi.Pia aliwaasa watu wenye ulemavu kutumia vipawa walivyojaaliwa na mwenyezi mungu kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao .
Aidha bi Ummy amemwambia mgeni rasmi kuwa Mradi huu wa kutoa vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu ulipatikana mwaka 2017 na ni wa thamani was kiasi cha shilingi milioni mia mbili unatekelezwa kwa awamu mbili ,awamu ya kwanza ni Mkoa wa Dar es salaam na Pwani na awamu ya pili ni Mkoa wa Morogoro na Dodoma na una lengo la kuwafikia watu wenye ulemavu wapatao 2050 msaada utakaojumuisha Try cicle 150,Wheelchairs 350 na white Canes 1550 na mpaka sasa mradi umefanikiwa kuwafikia wanufaika 695 wakiwemo wa Wilaya ya Kigamboni,Ilala,Temeke,Ubungo na Kinondoni jijini Dar es salaam.
Wakati anahutubia hadhara iliyojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo mgeni rasmi Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI amesema kuwa jamii kwa ujumla inatambua changamoto walizonazo watu wenye ulemavu na inawathamini kwa mchango mkubwa unaotolewa na watu hao.
‘’Serikali inatambua na kuthamini mchango na juhudi kubwa zinazofanywa na watu wenye ulemavu,na tumekuwa na viongozi wengi wenye ulemavu ambao wamepata fursa ya kulitumikia Taifa katika Nyanja mbalimbali kwa ufanisi mkubwa na bado Serikali inaendelea kuwajali na kuwatambua kwa mchango wao.Hivi karibuni Serikali imetangaza ajira zaidi ya elfu sita kwenye sekta ya afya na ninawaahidi watu wote wenye ulemavu kuwa wenye sifa wote wataajiriwa kwa asilimia mia moja,pamoja na ajira upande wa elimu wote kwa pamoja wataajiriwa’’ amesema Mhe. Selemani Jafo.
Katika zoezi hilo ambalo pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Evarist Ndikilo,Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Happiness Seneda , Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Zainabu vulu, Katibu tawala ndugu Mtela Mwampamba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mhe.Hamisi Dikupatile ,madiwani na Wataalamu wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Mussa Gama pamoja na wananchi waliojitokeza kwa wingi. By dkambanyuma.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa