Na
Mwandishi Wetu,
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka tarehe 16 Juni baada ya kupitishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU). Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Umoja wa Afrika imekuwa ikiadhimisha siku hii tangu mwaka 1991. Lengo la kuadhimisha siku hii ni kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976 walipokuwa wakiandamana kwa amani kupinga utawala wa kibaguzi uliokuwa ukiendeshwa na makaburu.
Watoto wa halmashauri ya wilaya ya kisarawe wameungana na wenzao kuadhimisha siku hii yenye kauli mbiu "Zingatia Usalama Wa Mtoto Katika Ulimwengu Wa Kidigitali" na kutumia fursa hii kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu malezi, makuzi, matunzo ulinzi na usalama wa watoto.Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya TRC Chanzige huku mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe. Fatma Nyangasa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya kisarawe amegusia suala la matukio ya ukatili wa kijinsia wanayofanyiwa watoto na amewataka watoto kutoa taarifa haraka wanapokutana na vitendo vya ajabu“Viongozi wa serikali walimu wanafanya jitihada za kuhakikisha haki za watoto zinalindwa hivyo wazazi na walezi tujitahidi kutengeneza ukaribu kwa watoto yetu ili wapate fursa ya kuwa huru kutuambia chochote anachokiona hii itasaidia kuhakikisha kwamba tunawalinda watoto wetu"
Vilevile amegusia juu ya utumiaji wa simu unavyoweza kuathiri mmomonyoko wa maadili kwa watoto hivyo amewasihi watoto wakisimamiwa na wazazi/walezi kusoma kwa bidii ili taifa lipate vijana bora kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa