WAZIRI DKT JAFO ATOKWA NA MACHOZI YA FURAHA AKIFUNGUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA DOLOLO AONGOZA DUA YA KUMUOMBEA RAIS DKT SAMIA
KISARAWE PWANI
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira MHE DKT SELEMANI SAIDI JAFO leo 04.01.2024 amefungua mradi mkubwa wa maji Kata ya mafizi Kijiji Cha Dololo uliogharim Shilingi 263,807,988.20.
Akizungumza wakati ziara ziara ya kukagua miradi mbalimbali ilikua ipo hatua za kukamilika kutoka idara ya afya na elimu na maji amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya mradi huo kukamilika,
"Ndugu zangu Wanakisarawe niongee kutoka moyoni kwa kumtanguliza Allah sw Nimefurahi Sana leo hapa Dololo kufungua mradi huu ambao mwaka 20.02.2022 ulianza Kupitia programu ya fedha za Maendeleo ya kupunguza adhari za ugonjwa wa UVIKO-19 alifafanua MHE DKT JAFO
Aidha kwa upande mwengine Meneja wa RUWASA wilaya kisarawe Eng Evangelist Kahwili alifafanua kuwa mradi huo una tenki la maji wenye ukubwa wa mita za ujazo 25 kwenye mnara wenye mita 12 pamoja na Bomba kuu lenye kusafirisha maji kwa tenki la mita 350 kwa kusambaza maji mita 3490 pamoja na kufunga pampu 2 za umeme wa jua alisisitiza ENG EVANGELISTA
Aidha kwa upende mwengine mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm kisarawe KOMRED KHALIFANI SIKA alimshukuru Mbunge kwa Kitendo Cha kutekeleza ilani ya chama kwa Vitendo maana Mambo mengi na yote yanatekelezwa kwa wakati alifafanua KOMRED SIKA,
mwisho katika ziara hiyo ya kukagua na kutembelea miradi ya pamoja na kuangalia jinsi mfuko wa Jimbo unavyofanya kazi MHE DKT JAFO aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtedaji Halmashauri Ndg DEOGRATIUS LOKOMANYA na kumuagiza asimamie kwa wakati ahadi alizotoa kwa vijiji ambayo vina miradi na ameahidi kutoa kutoka mfuko wa Jimbo,
Mwisho kaimu mkurugenzi Mtedaji Halmashauri Ndg DEOGRATIUS LOKOMANYA aliahidi kutekeleza ahadi ya MHE DKT JAFO ambayo ameahidi kwa vijiji vya Chakenge,mitengwe,Gwata,Masimba na Dololo kwa wakati,
"Naomba kukuhakishia kuwa Yale yote uloagiza kwa ofisi ya mkurugenzi Mtedaji Halmashauri yatatelezwa kwa wakati na kwa Vitendo" alisema DEOGRATIUS LOKOMANYA
MATUKIO MBALIMBALI ya picha wakati wa Ziara ya kutembelea na kuzungumza pamoja na kukagua miradi ya afya, elimu,na maji ya Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira MHE DKT SELEMANI SAIDI JAFO leo katika Kata ya Mzenga, Mafizi aliambatana na Wataalamu kutoka Ofisi ya mkurugenzi Mtedaji Halmashauri, Ofisi ya RUWASA,Mkuu wa Wilaya pamoja na Tanesco
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa