Jafo asisitiza utunzaji wa miundombinu ya maji KISARAWE.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAMISEMI MHE SELEMANI JAFO amewataka wanachi wa KISARAWE kata ya Masaki kijiji cha Sungwi kuitunza na kuhifadhi miundo mbinu ya Maji Safi na Salama hasa kisima kirefuambacho kinajengwa kwa Gharama shilingi Milioni Kumi na Nne kwa ufadhili wa Shule ya FEZA na Taasisi TIMETOHELP zote za Dare-saalaam, Akizungumza katika Ghafla ya kutambulisha mradi huo wa maji safi na salama ya kisima kirefu cha kisasa Sungwi.
Mhe Jafo alisisitiza jamii hiyo kuutunza na kuulinda mradi huo pamoja na kuutumia kwa manufaa kama ulivyo kusudiwa ili kuleta tija kwa Jamii na kuwa saidia wanafunzi na akina Mama ili kutokufuata Maji Masafa Marefu,Maji safi na salama yamekua na changamoto nyingi kwa jamii yetu hii hasa kipindi hiki cha kiangazi hasa maeneo ya ,Milimani ambayo ndio jamii kubwa ya wakaazi wa sungwi wanaishi mashambani na kupelekea kupata maji kwa shida alisema Jafo Shule ya FEZA na Tasisi ya TIMETOHELP kwa pamoja imetoa jumla ya milioni kumi na Nne kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya Kisima KIREFU kwa wilaya kisarawe kata ya Masaki kijiji cha Sungwi na Kifuru.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa