WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI MHE SELEMANI JAFO asisitiza ukamilishaji wa miradi ambayo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika jimbo la Kisarawe hasa katika sekta ya Afya, miundombinu ya barabara, ufugaji, kilimo, ardhi, ujenzi na elimu. Mhe. JAFO alisisitiza hayo alipokua akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imepatiwa fedha zote za mradi na bado inasuasua kukamilika na kuagiza kukamilika kabla ya mwaka 2018 kuisha. Akitolea mfano wa mradi huo ambao haujakamilika ni ujenzi wa kituo cha afya cha Chole uliopo kijiji cha Chole Kata ya Chole. Aidha Mhe. JAFO ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Kisarawe kuhakikisha miradi yote ambayo imekamilika hasa barabara ya chole kihare na daraja la Titu kufunguliwa kwa wakati kabla ya mwaka kuisha
‘’ Nakuagiza mkurugenzi andaa utaratibu wa kukamilika na kufunguliwa miradi hii haraka iwezekanavyo’’ alisisitiza Mhe Jafo. Fedha nyingi zimetumika katika mwaka wa fedha wa 2018 kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo katika wilaya ya kisarawe ambayo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ambayo msimamizi wa ilani hiyo ni Mbunge wa Jimbo .
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa