WIKI YA UNYONYESHAJI KISARAWE YAFANIKIWA.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE IMEZINDUA WIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI KATIKA KIJIJI CHA MITENGWE KATA YA MZENGA WILAYA YA KISARAWE.
KATIKA MAADHIMISHO HAYO YALIYOHUDHURIWA NA MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA KISARAWE ALIYEWKILISHWA NA AFISA TAWALA WA WILAYA YA KISARAWE NDUGU MTELA MWAMPAMBA YALIYOHUDHURIWA NA WANANCHI WENGI YALIFANA KWA KIASI KIKUBWA AMBAPO SHUGULI MBALIMBALI ZILIFANYWA
AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUMKARIBISHA MGENI RASMI,MGANGA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE BI ELIZABETH OMING’O AMESEMA MAADHIMISHO HAYA YANALENGA KUIHAMASISHA JAMII KUHUSU UNYONYESHAJI WA WATOTO ILI KUPUNGUZA UTAPIAMLO,VILE VILE YANALENGA KUIAMASISHA JAMII KUJITOKWZA MAPEMA KUTUMIA HADUMA ZA KLINIKI YA MAMA ,BABA NA MTOTO.
AIDHA MGANGA MKUU BI ELIZABETH AMESEMA SHUGHULI ZINAZOFANYIKA WAKATI WA MAADHIMISHO HAYA NI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UNYONYESHAJI,KUTOA CHANJO KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO,KUTOA CHANJO KWA WANANWAKE WENYE UMRI WA KUZAA KUANZIA MIAKA KUMI(15) NA TANO HADI AROBAINI NA TISA (49).
PIA KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI IDARA YA AFYA WILAYA YA KISARAWE IMEFANIKIWA KUTOA CHAKULA KWA WATOTO WENYE UTAPIAMLO,KUTOA MATONE YA VITAMINI A NA DAWA ZA MINYOO KWA WATOTO WENYE UMRI KUANZIA MIEZI SITA (6) HADI 59. NA KUTOA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO KWA WANAWAKE WENYE UMRI WA KUZAA.
BI ELIZABETH ELIZABETH OMING’O AMEONGEZA KUWA HUDUMA NYINGINE ZINAZOPATIKANA NI PAMOJA NA UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI NA SARATANI YA MATITI,KUTOA HUDUMA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO,UPIMAJI WA MAAMBUKIZI YA UKIMWI,KUTOA USHAURI KUHUSU NAMNA YA KUJIKINGA ,KUFANYA UCHUNGUZI WA KIFUA KIKUU KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO PIA KUTA ELIMU KUHUSU HAKI ZA WATOTO,ELIMU YA AFYA KWA MAKUNDI NA KUHAMASISHA JAMII KUJIUNGA NA CHF NA UPIMAJI MALARIA.
SHUKRANI ZA KIPEKEE ZIWAENDEE KOREA FOUNDATION FOR INTERNATIONAL HEALTHCARE (KOFIH) AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WAMEFANIKISHA MAADHIMISHO HAYA NA SHUKRANI ZA DHATI ZIWAENDEE PLAN INTERNATIONAL NA FEED THE CHILDREN AMBAO MARA KWA MARA WAPO BEGA KWA BEGA KATIKA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO WILAYANI KISARAWE
WILAYA YA KISARAWE KUPITIA IDARA YA AFYA IMEFANYA MAADHIMISHO HAYA KATIKA VIJIJI VYA MITENGWE,GWATA,MSANGA NA MLEGELE AMBAPO WANANCHI WAMEWEZA KUPATA HUDUMA ZA AFYA BURE .
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa