Ziara ya takribani siku tano aliyofanya Waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo La kisarawe Imeleta Hamasa kubwa na matumaini kwa wananchi wa Kisarawe ambapo mwanga mpya wa matumaini umejitokeza kwa wananchi hao.
Katika ziara hiyo iliyofanywa kwenye Kata za Marui,Msanga,Mafizi Vihingo na Kibuta ilihusisha vijiji kumi na mbili ambapo Mheshimiwa Waziri alifanya mikuatano kwa kukutana na wananchi wa vijiji hivyo kwa kuwaeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ,Mafanikio na changamoto zilizopo pamoja na kusikiliza kero,maoni na ushauri kutoka kwa wananchi hao.
Mheshimiwa selemani Jafo amewaeleza wananchi juu ya adhma ya Serikali kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo ili wananchi wanufaike kutokana na kodi zinazokusanywa na serikali kwa kujenga miundo mbinu na kuwaletea wananchi huduma mbalimbali.
“ Wananchi wa Kisarawe mmenipa dhamana ya kuwatumikia lakini Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania John Pombe Magufuli ameniona na kunipa dhamana kubwa ya kuwatumikia wananchi wa Nchi nzima na mimi ninawambia sitawaangusha.Tumeamua kutekeleza ilani ya Chama chetu Cha Mapinduzi kwa vitendo na sisi tuliopewa dhamana tumeamua kutekeleza kwelikweli,kwenye sekta ya Afya tumejenga miundo mbinu ya kuwezesha tunapeleka huduma za afya karibu na wananchi.tumejenga vituo vya Afya,Zahanati na tumepeleka magari ya wagonjwa sehemu mbalimbli za Wilaya yetu kwani kila kituo cha Afya kina gari ya kubebebea wagonjwa” amesema Mheshimiwa Jafo.
Aidha Mbunge wa Kiasarawe ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI amewaambia wananchi kuwa juhudi zinaendelea kufanywa katika sekta nyingi kama vile Elimu kwa Wilaya ya Kisarawe Miradi mingi imefanyika kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kujenga madarasa ,Nyumba za Walimu na vyoo ambapo Shule za Mitengwe,Boga, Kitonga Mango,Chang’ombe, Gwata Kwala na Yombo Lukinga zimejengwa Madarasa ya Kisasa pamoja na Ofisi za Walimu.
Pia katika ziara hiyo Mheshimiwa mbunge amewaambia wananchi kuwa jitihada kubwa zinafanywa na zinzendelea kufanywa katika sekta ya miundombinu ya Barabara ambapo barabara nyingi zimejengwa na kukarabatiwa ambapo Kwa Kisarawe mjini Barabara za lami zimejengwa kwenye mitaa na barabara zinazounganisha kata na vijiji zimekarabatiwa.
“ Katika ujenzi wa barabara ya kutoka Kisarawe hadi Maneromango ambayo ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi tumeanza kuijenga kwa kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tumemaliza kilomita sita za awali na sasa tunaendelea na ujenzi wa kilomita nne na hivi karibuni tumepata kiasi cha shilingi bilioni mbili amabazo tunaziingiza kwenye ujenzi wa barabara hiyo lengo kubwa tuweze kukamilisha ujenzi wa barabara ya lami kufika Maneromango inakamilika “ Aliongeza Waziri wa TAMISEMI.
Ziara ya Mbunge wa kisarawe iliweza kumfikisha katika vijiji vya Marui Ngwata na Marui Mipera katika Kata ya Marui ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa barabara kutoka kijiji cha Msanga hadi Marui barabara ambayo imekamilika pamoja na kukgua zahanati ya Marui Ngwata ambayo inatoa huduma kwa sasa.Pia alitembelea vijiji vya Ving’andi,Gwata na Mafizi katika kata ya Mafizi na vijiji vya Chamalale,Sangwe na Kibwemwenda katika Kata ya Vihingo na kuhitimisha ziara yake kwa kuzuru vijiji vya Mtamba, Masanganya na Bwama katika kata ya Kibuta.
Ziara hiyo iliyochukua takribani siku tano kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 21 mwezi wa tisa iliambatana na Msafara wa Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia na Afisa Mipango na Takwimu Ndugu Patric Allutte pamoja na Wakuu wa idara za Elimu Msingi Ndugu Esther Senkoro,Elimu sekondari NDUGU Kangisi,Afisa Mifugo,Afisa Kilimo,Afisa Maendeleo ya Jamii,Mhandisi wa Ujenzi,Afisa Ardhi,Mganga Mkuu wa Wilaya, Afisa Habari Ndugu David Kambanyuma,Mhandisi wa TARURA Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kisarawe na Wataalamu kutoka Ofisi ya TARURA Makao Makuu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Barabara mijini na vijijini.
Mbunge wa Kisarawe pia aliambatana na ujumbe kamili wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Wilaya Ndugu Halfani SIka,katibu wa Chama Wilaya.Katibu Mwenezi, Mwenyekiti wa umoja wa Vijana.Mwenyekiti wa Jumuija ya Wazazi, Mhamasishaji wa vijana pamoja na Katibu wa Mbunge .
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa