Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Nickson Simon John tarehe 25.06.2021 amefanya ziara ya kutembelea wafugaji na kuwakabidhi hati za kimila. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Mwanana Msumi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mhe. Zuberi Kizwezwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mussa L. Gama, Diwani wa kata ya Mafizi Mhe. Yadhamen Jafari Nghonde, Mwakilishi wa Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Pwani Ndg. Fredrck Mrema, Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mabula K. Isambula, watendaji wa kijiji na mtendaji wa Kata,pamoja na timu ya watalaam wa Ardhi na Ufugaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Aidha katika zoezi la ugawaji wa Hati za Kimila kwa wafugaji mwakilishi wa kamishna msaidizi wa ardhi wa mkoa wa Pwani Ndg. Fredrick Mrema alisema Hati ni ukombozi na kusisitiza kuwa hati ni Mali.
Katibu wa wafugaji wilaya ya Kisarawe Ndg. Filipo Umundi alimshukuru Mgeni Rasmi (Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe) kwa hatua kubwa ya ugawaji wa Hati za kimila kwa wafugaji na kumuomba kuwa zoezi hilo la ugawaji wa Hati lifanyike kote kwani ni chachu kwa maendeleo.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. Mussa L. Gama alimkaribisha mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Nickson Simon John, na aliwapongeza wanakijiji cha mafizi kwa kupatiwa Hati. Ndg. Gama Alisisitiza kuwa waliopewa Hati wazingatie masharti ya Hati hiyo na kudhibiti uzururaji ovyo wa wanyama, pia alimtambulisha mfugaji bora ambaye anaiwakilisha vema kisarawe, Ndg. Gama aliendelea kwa kuainisha vema kwa mkuu wa Wilaya changamoto ya mpaka kati ya wilaya Kisarawe na Wilaya ya Kibaha, na kuelezea maadhimio yaliyofikiwa kuwa mipaka imerekebishwa, kilichobakia ni kutangazwa rasmi. Amewatoa hofu wanakisarawe.
Aidha Mkuu wa Wilaya aliwapongeza wana Mafizi na wafugaji waliopatiwa Hati 24 za kimila na pia kuwakumbusha kuwa Ardhi ndo hifadhi ya maisha na alisisitiza kuwa hifadhi bora ni ile ambayo imelindwa, kisheria na kufuata taratibu na kanuni, Mhe. Nickson alisema kuwa kama wafugaji wana hati na wamesajiliwa inajenga msingi mzuri kwa wafugaji, mana serikali itajua idadi ya mifugo na ukubwa wa ardhi waliopewa. Pia alisema kuwa mali yenye thamani ni ile mali inayotambulika, inaweza kulindwa na kuendelezwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alisititiza kuwa kila haki inaambatana na wajibu, amewaasa wafugaji kuheshishimu mipaka, amewaomba wafugaji kuelewana na kutatua migogoro kwa kuzungumza na si kugombana. Amewaahidi wana Mafizi kuwa vijiji takribani 35 ambavyo havijapata usajiri atavifanyia kazi pamoja na timu ya watalaam wa Ardhi, Pia Mhe. Nickson alizungumzia vema Kauli mbiu ya Malisho Maji na Masoko akisema kwa ujumla zinaunda “MMM”, na kusema serikali itapambana kuhakiksha Malisho yanapatikana, Pia alisema hatua ya kupata Hati inasogeza hatua ya pili ya kupata Masoko. Mhe. Nickson alisema anapenda taarifa na amesema mwananchi yeyote anaweza kumpigia.
Aidha Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya maeneo ya wafugaji na kuona miradi mbalimbali na baadhi ya maeneo ya malisho ya wanyama.
Zoezi la Ugawaji wa Hati lilihitimishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Mhe. Zuberi Kizwezwe, ambaye aliwakumbusha wananchi kuambatana na kufanya kazi kwa bidii na kuepukana na migogoro pia alimpongeza Diwani wa Kata ya Mafizi Mhe. Yadhamen Jamal Nghonde kwa juhudi zake katika Kata ya Mafizi.
Mhe. Kizwezwe aliwashukuru wana Mafizi na kuhitimisha zoezi hilo.
Imeandaliwa na kitengo cha TEHAMA na Mahusiano
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa