MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA KISARAWE NDUGU SABRA AFUNGA MAFUNZO YA ARO KATA JIMBO LA KISARAWE ASISITIZA UADILIFU NA USAFI
Leo tarehe 06 Agosti, 2025
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kisarawe ndg Sabra C Mwankenja amefunga Mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata 34 (ARO KATA) wa Kata 17 zilizopo jimbo la Kisarawe Wilaya Kisarawe,
Akizungumza wakati wa kufunga amewasisitiza Wasimamizi Hawa ngazi ya Kata kusimamia Sheria na taratibu kwani zoezi hili la kupiga kura ni Msingi wa Haki ya Kila mmoja.
![]() |
![]() |
![]() |
aidha amewasihi Maafisa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata zote 34 kuzingatia Viapo walivyo apa pamoja na maelekezo yanayotolewa,
"Nina uhakika mtakwenda kutimiza wajibu Kwa kufuata Yale yote mazuri ambayo mmevuna hapa kwenye mafunzo mliopata katika kufanikisha zoezi la kupiga Kura." Amesema Mwankenja
Semina hii imefanyika Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Kisarawe
Zoezi hili litafanyika kwa mujibu wa sheria, na kuratibiwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kauli mbiu ya zoezi hili ni
"*Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"*
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa