Saturday 19th, April 2025
@KISARAWEDC
Na
Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amekutana na waheshimiwa Madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe 20/6/2023 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Akizungumza katika kikao hiko Mhe. Kunenge ametumia fursa hiyo kupongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kupata hati safi ya ukaguzi na ametaka kuona hali halisi ya utekelezwaji wa miradi na kutatua changamoto za Wananchi na Watumishi wa Wilaya ya Kisarawe.Vilevile amewaagiza wasimamizi wa miradi kusimamia miradi yote vizuri na kuhakikisha inakamilika kwa wakati pia miradi iendane na thamani ya fedha iliyopangwa.
Aidha amegusia suala la mapato na kuagiza kuangaliwa kwa makini ili kujua vyanzo gani visimamiwe vizuri vitasaidia kuongeza mapato katika halmashauri ya Kisarawe "katika mapato fanyeni operation ili mjue sekta gani mkiiwekea nguvu na kusimamia vizuri itawapa tija zaidi"alisema Kunenge.
Nae Mkaguzi Mkuu wa nje wa Mkoa wa Pwani Bi. Mary Dibago amewaagiza Madiwani na wataalam kuhakikisha hoja zote ambazo hazijajibiwa zinajibiwa.Pia amewaagiza wataalam kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi ambayo haijakamilika ili itekelezwe.
Kwa upande wake katibu Tawala wa mkoa wa pwani Rashid Mchata ameshauri viongozi kuwa na mpango mkakati wa utekelezaji pia kumpa ushirikiano Mkaguzi wa ndani ili kuepuka kuzalisha hoja vilevile ameshauri kamati ya fedha ihakikishe kila hoja zinagaiwa kwa wahusika na wapewe muda wa kujibu hoja hizo ili yule atakaeshindwa achukue hatua mapema kabla ya kufika hatua ya baraza pia ameongeza kwa kusema "wasilisheni mwenendo wa kujibu hoja hizo katika ofisi ya mkuu wa mkoa,kuna wataalamu hivyo mtapata fursa ya ushauri wa kitaalam
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa